|
|||
|
|||
Young Catholic Students – TYCS ni
kikundi cha kitume ambacho wanachama wake ni wanafunzi. Chama hiki kipo
katika ngazi ya Sekondari na vyuo. TYCS inawapa mafunzo wanachama wake
ushujaa wa kuangali kuchunguza mazingira ya uaanafunzi na kumtangaza Kristo
katika mazingira hayo. Chama hiki pia huamsha vipaji mbalimbali vya wanachama
na kuwafanya watambue vipaji vyao na kuviendeleza. Kazi hii hufanywa kwa
maongozi ya Roho Mtakatifu. Pia huwapatia wanachama wake semina mbalimbali
za kiroho, makongamano na mafungo yatakayowafanya watafakari zaidi neno
la Mungu.
TYCS inajitokeza katika kila shule ya sekondari ambapo panawanafunzi wakristo. Kwanza uanza kama kikundi kidogo katika shule kisha ujumuisha kanda na hatimae jimbo na pia Taifa.
Jimboni Tanga, Chama hiki kilianzishwa na marehemu Padre. Gerald Smith mwaka 1970 Chumbageni Tanga. Tangu mwaka 1976 PadreJames Kweka amakuwa masimamizi wa chama hiki cha TYCS. Mwaka 1994 Pd. Titus Mdoe amechukua jukumu hili la kukilea chama hiki na pia kama mkurugenzi wa miito mpaka mwaka 2006 pale alipokwenda masomoni Marekani. Kazi hii ya kukilea chama hiki na kushughulikia miito ilikabidhiwa kwa Pd. John Zuakulu. Chama hiki cha TYCS kipo karibu katika kila shule na vyuo hapa Jiboni Tanga. TYCS imefanya mambo mengi Jimboni Tanga, hasa kuwaleta wanafunzi pamoja, kufahamiana na kuinua vipaji vyao. Baada ya kumaliza masomo yao, wana TYCS bado wameendelea kuwa mfano mzuri sana katika maisha kama wakristo. Wamekuwa mfano mzuri kwa wakristo wenzao.le of Christian life in their respective Churches. They participate well in all activities in the Church, for example in the choirs and other activities. |
|||