KANISA KATOLIKI TANGA

Radio Huruma (RH)

RADIO HURUMA. (TANGA DIOCESE MULTIMEDIA COMPANY LTD (TDMCL))

RADIO HURUMA IN FULL OPERATION

Bodi ya Radio

Ratiba ya matangazo

Mawasiliano na Radio Huruma

Picha na matukio

'103.6 MHz Radio Huruma FM, Faraja kwa Jamii'

Kituo hiki cha utangazaji kilianzishwa mnamo 24 Desemba 2007.

 

Studio No 2 on air lump

Min Towel for STL

On air Lump, Studio No 1

 

Matangazo haya yalianza na urushaji wa ibada ya misa ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas, ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Anthony wa Paduaathedral Church Chumbageni Tanga. Ibada hii iliongozwa na Mhashamu Askofu Anthony M. Banzi Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga Diocese. Siku hadi siku Radio Huruma imezidi kuimarika na kuwa chombo muhimu kwa wakazi wa Tanga kwa upande wa Elimu, na Burudani.

MALENGO YA RADIO HURUMA (RH)

Ni kuwaambsha wakazi wa Tanga kifikira hasa katika mambo yanayohusu maendeleo yao na pia kutangaza neno la Mungu. Radio Tanzania Dar Es Salaam ambayo kwa sasa inafahamika kwa jina la TBC Taifa, utangaza habari zinazohufu Taifa zima. Ni mara chache sana TBC Taifa hutangaza habari za Tanga na kwa ufupi sana. Tanga yapo mengi ambayo yanatakiwa kutangazwa, hili pia nimepelekea kuanzishwa kwa kituo hiki cha Radio Tanga. Radio Huruma itaangalia kwa undani kila siku mambo yanayohusu Tanga, shughuli za wakazi wa Tanga na kuimiza ujenzi wa uchumi kwa kila mkazi wa Tanga.

Radio Huruma hutoa elimu kwa wasikilizaji wake, kuwahabarisha, kuburudisha kuhamasisha umoja na amani, upendo, haki sambamba na kulitangaza neno la Mungu. Kwa kufanya hivyo Kanisa Tanga linakamilisha ile kazi inayofanywa na serikali katika mapambano ya umasikini, ujinga, maradhi na kuwaandaa watanzania kuwa watu wema. Radio Huruma inajitahidi kujenga jamii yenye kuzingatia misingi ya haki, amani na upendo.

KITUO KILIPO:
Kituo cha utangazaji kipo katika mji wa Tanga, katika Kanisa Kuu la Jimbo Chumbageni Tanga katika jengo linalojulikana 'Pwani House.'

MASAFA YETU:
Radio Huruma inasikika karibu eneo lote la Mkoa wa Tanga Region na mikoa ya jirani. Katika Mkoa wa Tanga ni pamoja na wilaya ya Tanga, Pangani, Muheza, Kilindi, Korogwe, Lushoto, Mkinga, Handeni. Nje ya Tanga ni pamoja na kisiwa cha Pemba na baadhi ya maeneo ya kisiwa cha Zanzibar, Nchi ya jirani ya Kenya katika maeneo ya mji wa Mombasa.

Hawa ni wafanyakazi waanzilishi wa kituo cha Radio Huruma

Fr. Richard Kimbwi (Mkurugenzi Desemba 2007 hadi Januari 2010)

Mr. Majisu Mwanamboka (Mfanyakazi tangu Desemba 2007 hadi Machi 2009)

Mr. Daudi Julian Liunga(Vipindi vya michezo na burudani Tangu Mei 2008 hadi Januari 2009)

Miss Veronika Mtangi (Mtangazaji Tangu Januari 2008 hadi Februari 2009)

Mr. Frank Odomali (Program Manager Tangu Januari 2008)

Miss Theresia Prosper (Vipindi vya watoto Tangu Mei 2008)

Mr. Richard Valentino (Mfanyakazi tangu Julai 2008)

Miss Janeth Sendenga (Vipindi vya wanawake Tangu February 2008 hadi Januari 2009

Mr. Azaria Mwimbe (Mfanyakazi tangu Desemba 2007)

Miss Joyce Kimwemwe (Mtangazaji Vipindi vya dini Tangu Desemba 2008)

Miss Lilian Lihame (Mtangazaji Tangu Mei 2008 hadi Januari 2009)

Miss Blandina ( Afya tangu April 2008)

 

Peter Mtulia (Mtangazaji tangu 2009)

Miss Einoth Morel (Secretary tangu 2008)

Miss Zawadi Kika (Mtangazaji Tangu April 2009 hadi Decemba 2009)

Miss Evelin Balozi (Mtangazaji Tangu 2008)